Kiungo wa Manchester City, Yaya Toure, ameondolewa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast ambacho kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Togo na Moldova.
Kwa mujibu wa BBC, Toure ameondoshwa kikosini kutokana na sababu za kifamilia.
Toure alikuwa anarejea tena kuitumikia timu yake ya taifa baada ya kufuta uamuzi wake alioutoa 2015 kipindi cha Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika wa kutaka kustaafu kuichezea.
Ivory Coast itakuwa na kibarua dhidi ya Togo Machi 24 na dhidi ya Moldova 27 Machi 2018.
0 COMMENTS:
Post a Comment