March 17, 2018


Na George Mganga
 
Hatma ya klabu za soka kutoka Tanzania, Yanga na Simba kama zitasonga mbele kwenye michuano ya kimataifa itajulikana leo Jumamosi.

Baada ya Yanga kupoteza kwenye raundi ya kwanza dhidi ya Township Rollars FC kwa jumla ya mabao 2-1, leo itakuwa inarudiana na Wabotswana hao walio nyumbani mjini Gaborone.

Ili Yanga wasonge mbele wanapaswa kufunga mabao 2-0 au 3-1 ndiyo wapate nafasi ya kuendelea na mashindano.

Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utaanza saa 10:45 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Mbali na Yanga, Simba nao wana kibarua kingine cha marudiano kwenye Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry usiku wa leo.

Simba watakuwa wanahitaji ushindi wa bao moja pekee au sare ya 2-2 ili wajitengenezee mazingira ya kuendelea na michuano.



Katika mechi ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam, matokeo yalikuwa ni sare ya mabao 2-2 .

Mechi hii ya itaanza majira ya saa 2:30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Salehjembe.blogspot.com inaungana na watanzania wote kwa ujumla kuzitakia kheri klabu hizi ziweze kusonga mbele.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic