LIVE KUTOKA UWANJA WA TAIFA: MPIRA UMEKWISHA, YANGA 3-1 STAND UNITED
FULL TIME, Mpira umekwisha, Yanga wanaibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stand.
Dak ya 92, Mwamuzi wa kati anapuliza filimbi kumaliza mpira
Dak ya 91, Stand wako langoni mwa Yanga, kona inapigwa
DAKIKA 3 ZIMEONGEZWA
Dak ya 90, Bigirimana anakosa yeye na Rostand, bahati si nzuri kwa Stand
Dak ya 89, Yanga wanapata kona kufuatia shambulizi kali walilolipata, bado upo langoni mwa Stand, wanaokoa sasa.
Dak ya 87, Stand wanaanza tena lakini Juma Mahadhianacheza faulo, inapigwa hatari huku, mpira unakwenda nje.
Dak ya 85, Chirwaaaa, anafunga bao la 3, Yanga 3, Stand United 1
Dak ya 84, Goooli Stand United wanapata bao la kwanza
Dak ya 82, Buswita na mpira, anapaia kulia kwake Martin, bado wanao Yanga. Unapigwa kwake Chirwa, dakika zinazidi kuyoyoma.
Dak ya 81, Stand wanapata nafasi nyingine ya kufunga lakini kipa Rostand anauwahi mpira, anaanza upya.
Dak ya 80, Zimesalia dakika 10 pekee mpira kumalizika
Dak ya 77, Mpira anao Rostand, anaupiga mbele na kuwafikia mabeki wa Stand, kwake Blaise, inapigwa krosi kali lakini inakosa mtu wa kumalizia na mpira unatoka nje.
Dak ya 75, Ndikumana anakosa nafasi ya kufunga bao, mpira unakata mguu na kwenda nje.
Dak ya 74, Chenga za Chirwa zisizo na maana zinaigharimu Yanga kukosa nafasi ya kufunga goli la 3, mabeki wa Stand wanaondoka na mpira.
Dak ya 72, Stand wanapambana kusaka goli la kwanza, bado wanaumiliki mpira, kona kuelekea Yanga.
Dak ya 71, Buswita anapata kadi ya njano, matokeo bado ni 2-0.
Dak ya 68, Faulo nyingine inapigwa kuelekea Yanga, anapiga Aaron Lulambo, inakwenda nje.
Dak ya 64, Linapigwa shuti kali langoni mwa Yanga na kugongwa mwamba, mpira unarudi ndani, nafasi wamekosa Stand ya kuandika bao hapa
Dak ya 63, Stand wameamsha mashambulizi sasa, wanapasiana kuelekea mbele, inapigwa krosi kushoto wa Uwanja, kipa Rostand anadaka.
Dak ya 61, Faulo nje kidogo ya 18, inapigwa kuelekea langoni mwa Yanga, kama Stand wakitulia wanaweza kupata bao, inapigwaa, kipa anapangua na mpira unaokolewa.
Dak ya 60, Hatari katika lango la Yanga, mabeki wanaokoa
Dak ya 58, Bado mpira umesimama, Rostand ndiyo ananyanyuka sasa.
Dak ya 56, Mpira umesimama kwa muda, Rostand ameumia, anagangwa uwanjani.
Dak ya 55, Stand wanafanya shambulio kali huku, inakuwa kona, kona inapigwa inamkuta Bigirimana anapigwa kichwa lakini mpira unaokolewa.
Dak ya 54, Buswita sasa na mpira, inakuwa faulo kwenda Stand.
Dak ya 53, Mpira sasa anao Blaise, anakwenda huku, faulo, inapigwaaa lakini inakwenda nje
Dak ya 52, Ibrahim Ajib anaumia, anatolewa nje kwenda kugangwa, mabao bado ni 2-0.
Dak ya 50, Stand sasa wanapandisha mashambulizi, wanapasiana kati mwa Uwanja, inapigwa mbele huku kwake Ndikumana, anapiga kroosi, nje.
Dak ya 49, Ndikumaaana, ametengenezewa pasi nzuri hapa, lakini shuti lake la mguu wa kushoto linakwenda nje
Dak ya 47, Hatari langoni mwa Yanga, inapigwa krosi na mshambuliaji wa Stand lakini Mwamuzi wa pembeni ananyoosha kibendera kuwa mpira ulikuwa umeshatoka.
Dak ya 46, Pisu Buswita anapata nafasi nzuri nje ya 18, anapiga shuti lakini linakwenda nje, Stand wanaanza
Dak ya 45, Kipindi cha pili kimeanza.
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zimemalizika, Yanga wanatoka kifua mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya Stand United, Wafungaji ni Yusuph Mhilu (6') na Ibrahim Ajib (11')







0 COMMENTS:
Post a Comment