Stand United itakuwa ina kibarua dhidi ya Njombe Mji katika Uwanja wake wa nyumbani, CCM Kambarage, mchezo utakaoanza saa 10 kamili jioni.
Baada ya mchezo huo siku ya Ijumaa, ratiba itaendelea tena Jumamosi ya Machi 31 2018 kwa mechi mbili ambapo Tanzania Prisons itaikaribisha JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya huku mechi ikianza saa 8 kamili mchana.
Siku hiyohiyo Azam FC itakuwa inacheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex, mchezo utaanza saa 2 kamili za usiku.
Hatua hiyo ya robo fainali itakamilika Jumapili, April 1 2018 kwa mchezo mmoja kuchezwa Uwanja wa Namfua kati ya walima alizeti, Singida United watakaokuwa nyumbani dhidi ya Yanga.








0 COMMENTS:
Post a Comment