TSHISHIMBI ATANGAZWA KUWA MCHEZAJI BORA LIGI KUU MWEZI FEBRUARI, AWAPIKU OKWI NA BUSWITA
Na George Mganga
Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kupitia Bodi ya Ligi, limemtangaza Mchezaji, Kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Februari.
Tshishimbi ametwaa tuzo hiyo baada ya kuisaidia timu yake kuvuna alama 12 huku akifunga mabao matatu na akitengeneza moja.
Mechi ambazo Tshishimbi alihusika kwenye ushindi katika mwezi Februari ni dhidi ya Majimaji, Njombe Mji, Ndanda na Lipuli ya Iringa.
Pius Buswita (Young African) na Emmanuel Okwi (Simba SC) ni wachezaji ambao waliokuwa kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hiyo kwa mwezi huu wa pili.
Tshishimbi ambaye ni mshindi wa tuzo hii, atazawadiwa kitita cha milioni moja sambamba na king'amuzi cha Azam TV.








0 COMMENTS:
Post a Comment