OKWI NA BOCCO FITI ASILIMIA 100 KUKIPIGA DHIDI YA AL MASRY JUMATANO, UFAFANUZI WA HALI ZAO KIAFYA UPO NAMNA HII
Na George Mganga
Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi, ametajwa kucheza mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho ambao Simba wataikabili Al Masry SC ya Misri, Jumatano ya wiki lijalo.
Okwi ambaye aliumia katika mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC na kupelekea kutolewa nje huku nafasi yake ikichukuliwa na Laudit Mavugo, hali yake kwa sasa inaendelea vizuri na kufikia Jumatano atakuwa fiti kucheza.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema Okwi atacheza mchezo huo.
Mbali na Okwi, Manara amesema pia, mshambuliaji wao aliyeumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC, John Bocco, atakuwepo katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho kutokana na hali yake kuendelea vema hivi.
Bocco amekosekana katika mechi zaidi ya mbili ambazo ni dhidi ya Mbao FC na Stand United, pia Gendarmarie Nationale FC kutokana na majeruhi.
Ujio wa wachezaji hao ndani ya Simba unaweza kuleta manufaa kutokana na namna ambavyo wamekuwa wakiihimili safu ya ushambuliaji ndani ya kikosi chao.
0 COMMENTS:
Post a Comment