NIYONZIMA AREJEA NCHINI, NI BAADA YA MATIBABU KUKAMILIKA
Na George Mganga
Taarifa kutoka kwa uongozi wa klabu ya Simba zinaeleza kuwa kiungo, Haruna Niyonzima tayari amesharejea nchini baada ya matibabu yake kukamilika huko India.
Haruna alisafiri kuelekea India kwa ajili ya kufanyiwa operesheni ndogo kwenye mguu wake baada ya majeruhi ambayo yalimfanya asionekane Uwanjani na kikosi kwa muda mrefu sasa.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesema kuwa Niyonzima alipaswa kufanyiwa operesheni lakini haijawa hivyo lakini amesganyiwa matibabu ambayo yamemfanya arudi katika hali yake ya kawaida.
"Niyonzima amesharejea nchini, hali yake sasa iko vizuri, tulitarajia atafanyiwa opereshi lakini haijawa hivyo, japo ametibiwa bila operesheni kufanyika" amesema Manara.
0 COMMENTS:
Post a Comment