March 13, 2018




Kikosi cha Simba, kinatarajia kutua nchini Misri kesho Jumatano saa tatu na ushee usiku.

Baada ya kutua, Simba italala jijini Cairo, italala hapo na kufanya mazoezi siku itakayofuata kabla ya kuanza safari ya Port Said Ijumaa.

Ingawa imeelezwa, ratiba hiyo inaweza kubadilika kulingana na watu wa Simba waliotangulizwa nchini Misri kwa ajili ya maandalizi.

Simba inajiandaa kuivaa Al Masry katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho itakayopigwa Jumamosi.

Msemaji wa Simba, Haji manara amesema maandalizi ya safari hiyo yamekamilika na waliotangulia jijini Cairo wamekuwa wakiendelea na maandalizi.

Katika mechi ya kwanza, Simba ilipata sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

1 COMMENTS:

  1. Msemaji anasema kesho alfajir wewe kesho jion..duuuuuu sis tunamwamin msemaji wa tim sijui Habarisource zako nizp mana si Leo tuu inagawa tunaitegemea sana blog yako hii

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic