Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi jioni hii katika Uwanja wa Boko Vetarani uliopo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.
Simba wanajiandaa na mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry SC kutoka Misri. Mchezo huo utafanyika huko Misri, Machi 17 2018.
Mechi ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2, hivyo Simba watalazimika kwenda kushinda ugenini ili wapate nafasi ya kusonga mbele.
Taarifa kutoka ndani ya wekundu hao wa Msimbazi, zimearifu kuwa kikosi chao kitaondoka nchini Jumatano ya wiki hii kuelekea Port Said, Misri, kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano.








Simba wanaboa sana cjui tatizo lao nn ,ifikie hatua baadhi ya mabeki waambiwe ukweli waache kucheza kimazoea LA sivyo kila anayesababisha goli au kuwa chanzo cha timu kufungwa akatwe mshahara haiwezekani tatizo LA kurudishwa magoli liwe kwetu tu,tunashinda hata haichukui muda magoli yanarudi huu ni ujinga na ushenzi na sijasikia kiongozi wala kocha kuzungumzia hili,kipindi cha nyuma lilipotea limerudi tena why huu ujinga,basi Mbonde aanze na viungo waimarishwe
ReplyDelete