March 14, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), limemteua kwa muda, Ammy Ninje, kuwa Kocha wa muda wa Timu ya taifa ya Vijana wenye chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes.

Ammy Ninje ametangazwa leo na Shirikisho hilo ili kuiandaa Ngorongoro Heroes kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Morocco na Msumbiji ikiwa ni kabla ya kucheza na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuelekea AFCON U20.

Ngorogoro Heroes itacheza na timu ya Taifa ya Vijana ya Morocco Jumamosi ya Machi 17, 2018 na dhidi ya timu ya Taifa ya Vijana Msumbiji, Jumatanoya Machi 21, 2018. Michezo yote ikichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON U20, Ngorogoro Heroes itacheza dhidi ya DR Congo Machi 31 katika uwanja wa Taifa, na mchezo wa marudiano kufanyika baada ya wiki mbili jijini Kinshansha Congo DR.

3 COMMENTS:

  1. Huyu cocha wanampendea nn c juz juz tu alivurunda anamafanikio ypi kwny taalum ya ukocha!

    ReplyDelete
  2. Hii sio ttf bali ni kichefuchefu.Ujinga mtupu uliojaa ubabaishaji. Sijui watanzania alieturoga ni nani kila kitu kwetu ni mzaha mzaha. Hata Kuabudu Mungu pua ni kwa mzaha mzaha. Kula kwetu ni kwa mzaha mzaha. Hakuna tulipokuwa serious tukatajwa na Dunia watanzania kwa jambo fulani achana nao. Labda watanzania tupo serious katika kujidumaza.Wao TTF kama wameshindwa kutafuta makocha kama kutafuta makocha wa ukweli wa kujenga misingi imara ya timu ya taifa waseme tu sisi tutawatafutia kocha wa maana hata bure. Huwezi kuwa na zamira ya kuinua jengo imara bila ya kupata mifano ya kazi ya fundi unaetaka kumuajiri. Labda uwe hujui nini unachokifanya na umeamua kubahatisha lakini tarajia kuja kujuta baadae. Labda TFF wamemchagua huyu kocha kwa kuwakomoa wale wote waliowasema vibaya wakati walipompa timu ya Taifa kule kenya. Vipi Suleiman Matola alishafanya kazi nzuri sana pale simba ya kuwaketa akina Said Ndemla na wenzke ana uzowefu tayari na tabia na hulka za makuzi ya soka la vijana wa kitanzania. Huo mfano wa Matola ni mmoja tu lakini kuna wengi nnaimani wenye uwezo na sifa walistahili kupewa majukumu ya kujenga vijana wa timu ya Taifa ya kesho kuliko kupewa mtu asijulikana historia yake.

    ReplyDelete
  3. CV ya Ammy Ninje ikoje? Katokea wapi au ndio yule aliyetika Uingereza ambaye alishindwa vibaya na kututia aibu timu yetu? Mnaomjua vizuri Ammy Ninje? Au kuna mchezo wa hovyo hapa unafanyika TFF ?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic