WANAOMLAUMU AMMY NINJE SABABU YA KIINGEREZA WANAPASWA WAJITAFAKARI UPYA
Na George Mganga
Kocha wa Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje, ameanza safari nzuri kuelekea mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika chini ya miaka ishirini (AFCON U20).
Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa mwezi Machi 31, 2018 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Saalam, hiyo itakuwa ya mkondo wa kwanza.
Mkondo wa pili utafanyika baada ya wiki mbili baadaye jijini Kinshasa, Congo.
Kejeli na minong'ono naweza kuisema haswa kwa watu ambao hawana uelewa ilianza kumfikia Kocha Ninje wakati akitangazwa na utawala huu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kuifundisha Kilimanjaro Stars.
Ninje alikabidhiwa Kilimanjaro Stars kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Chalenji iliyofanyika nchini Kenya Disemba mwaka jana.
Kikosi hicho kilichoenda kushiriki mashindano hayo, kiliambulia sare mchezo mmoja na kufungwa miechezo mingine kisha kutupwa nje ya CECAFA.
Achana na kutofanya vizuri kwa Kilimanjaro Stars, Kocha Ninje amekuwa akitupiwa lawama, kejeli na majungu tangu kipindi hicho anakabidhiwa Kilimanjaro Stars.
Si tu mashabiki, bali hata baadhi ya wadau wa soka wamekuwa wakimtupiwa lawama sababu tu, ya kuzungumza lugha ya Kiswahili huku akichanganya na Kiingereza wakati akiongea na Waandishi wa Habari, au akihojiwa.
Kiingereza kuwekuwa kama kama tatizo kubwa na mpaka imefikia baadhi ya mashabiki na wadau wa soka kuanza kuhoji iweje Mwalimu huyu azungumze Kiingereza.
Nadhani tatizo kubwa la Watanzania ni kutaka kumsikia Ninje akizungumza Kiingereza na kusahau kama binadamu tunaishi na kukua katika mazingira tofauti.
Watanzania hawahawa wanasahau hata baadhi ya wachezaji wakisafiri kwenda na timu nje ya nchi, baada ya mechi wakihojiwa wanshindwa kuzungumza vizuri hii lugha ya kigeni.
Inawezekana ikawa kuna tatizo la utambuzi na ufahamu ndani ya fikra, kwa baadhi ya wanaomponda ama kumsema kwanini anachanganya lugha.
Tunapashindwa hata kuelewa hawa wachezaji wakubwa wanaosakata kabumbu barani Ulaya, wengi wametokea kwenye mataifa tofauti, lakini hawajui lugha za kule wanapotumikia maisha yao ya soka lakini kazi nzuri wanaifanya Uwanjani.
Ni vema mtu tukamtupia lawama kwa kile anachokifanya endapo kinakuwa hakiendana na matakwa ya wengi na pia kinakuwa kina mtazamo chanya. Haki ya kuhoji kama Kocha ameshindwa kuisaidia timu ipate matokeo tunayo.
Hili la Kiingereza si sahihi, lugha haiwezi kusababisha timu kuwa na matokeo chanya, bali mipango na mikakati mizuri pamoja na ufundi wa Mwalimu ndiyo nguzo pekee ya kuifanya timu ifanye vema.
Tufikie hatua tujaribu kujitafakari kabla ya kutupia kitu lawama, si sahihi kumlaumu Ninje sababu anazungumza Kiingereza, tumrekebishe pale anaposhindwa kukimudu kikosi na pia kusifia pale anapofanya vizuri.
Mwandishi unajichanganya. Umewahi kumsikia Messi akizungumza Kiingereza? Wachezaji wetu kimsingi hawapaswi kukubali kuhojiwa kwa Kiingereza. Wanapaswa kuhojiwa kwa lugha wanayoielewa. Ni ulimbukeni wenu ndiyo unaowafanya mdharauliwe. Mnadhani kuzungumza Kiingereza ni usomi. Kama maisha yako hayakulazimishi kuzungumza Kiingereza, chanini kuking'ang'ania? Ninje ni Mtanzania. Anawasiliana na Watanzania. Anachanganya lugha ili iweje?
ReplyDelete