MSHAMBULIAJI wa Klabu Bingwa ya Azam FC, Yahya Zayd, ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa timu hiyo (NMB Player Of The Month) mwezi Januari-Februari.
Kwa mujibu wa Azam FC kupitia ukurasa wao wa Facebook, umeandika Zayd ametwaa tuzo hiyo akiwazidi wachezaji wenzake kwa kura.
Zayd ametwaa tuzo hiyo akiwazidi ambao ni Nahodha Msaidizi Agrey Moris na kiungo Salmin Hoza, baada ya mashabiki kumpigia kura 102 kati ya 144 zilizopigwa sawa na asilimia 70.8 huku Moris akipata 27 (18.8%) na Hoza 15 (10.4%).








0 COMMENTS:
Post a Comment