April 20, 2018



Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje, ameamua kuja kivingine kuelekea mchezo wa marudiano wa kufuzu kwenda mashindano ya AFCON chini ya miaka 20 kwa kuamua kuachana na mfumo wa Diamond.

Ninje ameeleza atatumia mfumo mpya ambao utaiwezesha Ngorongoro kupata matokeo katika mchezo huo utakaopigwa Kinshasa, Congo, Aprili 22.

Inaonekana dhahiri shahiri Ninje hatotumia tena mfumo wake aliouzoea wa Diamond baada ya kulazimishwa suluhu ya kutokufungana na Congo katika mechi ya awali iliyofanyika Dar es Salaam.

Tayari kikosi hicho kimeondoka jana nchini kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Congo ambayo ni muhimu zaidi kwa Ngorongoro kupata matokeo.

Hifadhi ya Ngorongoro imedhamini safari ya vijana hao kuelekea Congo kwa mujibu wa taarifa iliyotolea na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jana.

1 COMMENTS:

  1. Sisi watanzania mafundi sana wa kucheza na midomo yetu wacha tu tuendelee na majaribio yetu sijui lini tutakuwa serious?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic