April 18, 2018





Kipa wa Pretoria University ya Afrika Kusini, Deogratius Munish ‘Dida’ amese,a baada ya soka ambayo ni lazo yake, anafarijika zaidi kuumaliza muda wake akiwa kanisani.

Dida ameiambia SALEHJEMBE kutoka jijini Pretoria, Afrika Kusini kwamba anafurahia zaidi maisha ya kuabudu.

“Kila ninapomaliza kazi, ningependa kuwa kazini nikiabudu. Napenda sana maisha ya hivyo.

“Unajua kila mtu anakuwa na chaguo lake. Kazi ya soka mara nyingi ni mazoezini au maandalizi ya mechi.

“Kipindi cha mapumziko, wachezaji hupenda kupata kitu ambacho kinawafariji na mimi kanisani  ni sehemu sahihi kwangu,” alisema.

Dida amekuwa akiabudu katika Kanisa la South Africa Fellowship of Churches la jijini Pretoria, hali iliyomfanya kupata marafiki wengi ambao pia hujitokeza kuabudu katika kanisa hilo.

Kipa huyo wa zamani wa Yanga sasa amekuwa akipata nafasi ya kucheza katika kikosi hicho kinashiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Afrika Kusini.

Kabla, Dida alikaa nje kwa muda mrefu baada ya kuumia siku kadhaa baada ya kujiunga na timu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic