April 5, 2018




Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva, leo amewasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili akiwa sambamba na Makamu, Godfrey Nyange Kaburu.

Aveva amefika mahakamani hapo leo ambapo jana alipaswa kusomewa maelezo ya awali mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Licha ya kusomewa maelezo hayo, kesi hiyo imeahirishwa tena mpaka mwezi Aprili 12 2018 kufuatia Wakili wa TAKUKURU, Leonard Swai, kuomba hati ya mashtaka ifanyiwe mabadiliko.

Swai ameiomba Mahakama kubadilisha hati ya mashtaka kwa kumuongeza mshtakiwa mwingine ambapo Aprili 12 2018 watasomewa maelezo hayo ya awali.

Taarifa zinaeleza kuwa hatua hiyo imefikia hapo baada ya upelelezi kukamilika upande wa mashtaka.

Muhusika mwingine anayekabiliwa na kesi hiyo ni Makamu wa Rais wa Simba, Godfrey Nyange Kaburu ambaye alitinga pia mahakamani hapo leo.

Washtakiwa wote wawili wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi nyaraka za uongo na utakatishaji wa fedha, kiasi cha USD 300,000.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic