April 5, 2018



Licha ya kupokea kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Liverpool katika mechi ya mkondo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kocha Pe Guardiola amwagia sifa wachezaji wake.

Akizungumza baada ya mchezo kumalizika, Guardiola alisema wachezaji wake walicheza mchezo mzuri kwa kupambana vya kutosha huku akiahidi wanaweza wakalipiza kisasi mechi ya marudiano.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Dimba la Anfield katika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo, Liverpool ilijipatia mabao yake kupitia Mohammed Salah, Oxlade Chamberlain na Sadio Mane.

Mbali na matokeo hayo, Guardiola alimtupia lawama Mwamuzi aliyechezesha mechi hiyo, Felix Brych akisema kuna baadhi ya sehemu aliteleza kufanya maamuzi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic