April 10, 2018


Winga nyota wa zamani wa Simba na Yanga, Thomas Kipese ni kati ya “Wababa” waliopokea wito kwenda katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Lakini mwenye amezungumza na SALEHJEMBE na kusema barua hizo si kweli.

"Ile barua si ya kweli, unajua tunataniana na Bakari Malima, ametengeneza tu na kuweka pale kama utani sasa imesambaa sana," alisema.

Inaonekana Kipese amepokea wito akiwa kati ya baba au wazazi wa kiume wanaolalamikiwa. Ingawa yeye kasisitiza si sahihi ni utani.




Kinamama 480 wamejitokeza katika ofisi za Makonda wakiitikia wito wa kusikilizwa malalamiko yao kuhusiana na kutelekezwa.

Kipese, ameandikiwa barua na katibu tawala wa mkoa wa Dar es Salaam, kufika ofisini kwake kuhusiana na suala hilo la malezi ingawa barua hiyo haijafafanua ni mtoto au  watoto.
.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic