Na George Mganga
Kikosi cha Simba SC kinashuka dimbani Alhamis ya wiki hii kucheza na Mbeya City FC katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba inaingia kucheza mechi hiyo ya ligi huku wachezaji wake kadhaa wakitoka kutumikia adhabu ya kuwa na kadi tatu za njano kwa kila mmoja.
Beki Juuko Murushid, Erasto Nyoni na Kiungo James Kotei waliukosa mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar FC baada ya adhabu ya kutumikia kadi hizo kumalizika.
Tayari kikosi hicho kimesharejea jijini Dar es Salaam na sasa kinaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani uliopo pembezoni kidogo mwa jiji la Dar es Salaam.
Urejeo wa wachezaji hao utakuwa unaipa nguvu Simba ya kukiimarisha kikosi hicho ambacho kipo kileleni mwa msimamo wa ligi hivi sasa kwa kuwa na pointi 52.
0 COMMENTS:
Post a Comment