Vikosi vya Majimaji ya Songea na Njombe Mji FC, ndiyo vyenye hofu zaidi ya kuporomoka daraja.
Majimaji ambayo kihistoria ni kubwa, ndiyo inayoshika mkia ikiwa na pointi 16 na kuzibeba timu zote za Ligi Kuu Bara.
Inafuatiwa na Njombe mji ambaye ina pointi 18 katika nafasi ya 15 kati ya timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo.
Pamoja na timu hizo mbili, Mbao FC na Kagera Sugar zenye pointi 20 na 22, bado ni kati ya timu zilizo katika nafasi mbaya na zinatakiwa kufanya kazi ya ziada.
Tayari kila timu imecheza mechi 23, kila timu imebakiza mechi hizo saba ambazo ni “kufa au kupona”.
0 COMMENTS:
Post a Comment