KOCHA MTIBWA AKUBALI MATOKEO, KIFARU AGOMA KUPOKEA SIMU
Baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Simba SC jioni ya leo, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amekubali matokeo.
Akizungumza mapema baada ya mchezo huo kumalizika, Kocha Zubeiry Katwila, amesema kila timu imecheza kwa kupambana, lakini Simba wameweza kutumia nafasi yao.
Katwila ameeleza kuwa wachezaji wake walipambana na kutengeneza nafasi lakini hawakuweza kuzitumia vizuri na mwisho wa siku kupelekea kupoteza mchezo huo.
Mbali na Kocha huyo kuzungumza, Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru alishindwa kupokea simu yake baada ya mchezo kumalizika, yawekezekana ikawa ni presha ya matokeo.
Wa nje tulifuatilia pia kutokana mvuto wa pambano hilo. Ila kuna vitu ukiviona vinatia kichefuchefu. Sisi watanzania ni watu wa hovyo sana tena sana. Sisi watanzania ni wazembe kuliko wazembe. Ni wavivu kuliko wavivu. Ni wapuuzi waakili kuliko wapuuzi tusioijua thamani yetu yaani bongo zetu zimeoza kiasi kwamba kama ingekuwa spare parts basi mtu kama Magufuli labda kwa shirikiana na wataalamu wa nje ili apress order kwa ajili ya kuagiza bongo mpya ili kuja kupandikizwa katika vichwa vya watanzania. Nimekereka na kuvunjika tamaa baada ya kuona ile hali ya ule uwanja wa jamuhuri pale Morogoro. Inaonekana ule uwanja hauna mmiliki ? Wala wahusika wanaosimamia mpira au ligi pale Morogoro walikuwa hawajui kama ule uwanja utatumika kwa ajili ligi tena big mechi,kwa sababu tulimshuhudia Referee akikarabati nyavu za goli badala ya kupuliza filimbi ya kuanzisha mpira kama anavyotakiwa. Hali ya ule uwanja ni ya hovyo kabisa. Uwanja wa mpira sio sehemu ya kuchezea peke yake bali mazingira yake yote ya ndani na ya nje yanayouzunguka yanatakiwa yawe ya salama na ya kuvutia. Na mara nyingi matunzo yake wala hayahitaji mabilioni ya pesa kuweka mazingira safi ya uwanja zaidi ya nguvu kazi. Kuyapunguza au kuyakata majani yaliyozidi kimo yanayozunguka uwanja wala hayahitaji mamilioni? Kuziba sehemu ya matope inayozunguka uwanja wala sio big deal kwa watu wenye kuelewa nini faida ya kuishi katika mazingira bora. Sinahakika lakini uwanja wa jamuhuri Morogoro ni uwanja namba moja wa mkoa wa Morogoro na hahilisi nani anaumiliki. Ile pale ni aibu. Watanzania lazima ifike pahala tuwe watu wa kuona aibu. Timu zinaajiri makocha wa gharama kutoka nje ya nchi. Mechi zinarushwa kwenye matv na mitandao karibu duniani kote watu wanaangalia lakini ukiangalia mazingira ya viwanja Tanzania ni aibu. Viwanja hivi vingi vimekuwepo miaka nenda miaka rudi na kama kuungekuwepo na nidhamu na uadilifu katika udhibiti wa kidogo kinachopatikana kutokana na ada za viingilio hivi viwanja visingekuwa na hali mbaya Ile. Viwanja ni mabostani viwe vya maeneo ya wazi au ya ndani vinapaswa kuwa katika hali ya kupendeza. Lakini watanzania akili zetu bado zimelala sana bado tunahitaji watu wakutuamsha Magufuli peke hatoshi. Mzee wa watu anahangaika katika kuhakikisha watanzania wanaamka lakini ndio kwanza watu wanamuendea makinasani kuomba aachane na jitihada zake mapadri na waraka wao wamesibitisha hilo. Lakini tuache utani ili Magufuli afanikiwe lazima wapatikane angalau viongozi watatu wenye mshike mshike kama yeye mwenyewe au zaidi yake na ndio maana lawama zote za wale wasiotaka afanikiwe zinaelekezwa kwake kwa sababu yupo kama lonely soldier. Muheshimiwa raisi anatakiwa kufanya maamuzi magumu kutafuta wasaidizi wenye kuhangaika kama yeye mwenyewe binafsi wasiokuwa na muhali au wasaidizi wake wa sasa wanatakiwa kubadilika. Kazi kubwa kwa Tanzania ni kazi ya kuwazindua watanzania kutoka katika uzingizi na kuanza kujituma na kuthamini na kukitunza kile kidogo walichonacho kwani hata M'buyu ulianza kama mchicha. Ikiwa tunashindwa kuvitunza na kuviweka hivi viwanja vilivyopo sasa katika mazingira mazuri basi hata vikijengwa viwanja vipya itakuwa kazi bure.
ReplyDeleteMkuu usi generalize kutokana na upeo wako. Sisi wengine ni wabongo lakini hatuingii kwenye hilo group lako. Watu zaidi ya milioni 50 hawawezi kufananishwa kwa kupitia hiyo makala yako.
ReplyDeleteBrother Moudy lengo sio kukashifu au kujikashifu sisi wenyewe kama watanzania,bali lengo ni kutoa tanabahi kuonesha madhaifu yetu tena makubwa miongoni mwa watanzania tuliowengi.Kwa mfano ukichukulia kesi za akina Jamali Malinzi, Aveva, wambura, Watumishi hewa, wenye vyeti hewa, waliojiunganishia bomba la mafuta kuna wale waliofurahia ndege kuzuiwa kule Canada nakadhalika hapo utaelewa nawazumzia watanzania wa aina gani. Na nnaimani kubwa watumishi wengi wanaojishughulisha na mpira kama makocha na wengineo kutakuwa wapo wenye vyeti hewa kwani huko mkono wa serikali haujafika.
ReplyDeleteInabidi kwa kweli tubadilike.Rais Magufuli anajitahidi sana kutuongonza na kutuonyesha dira.Wakati Trump anatuambia from "shithole"tunatoa povu.Sijui tunatakaje?
ReplyDeleteReli ya kisasa inajengwa itakayowezesha treni toka D'salaam to Morogoro kwa saa moja na nusu.Hivyo Morogoro municipal council ndio inabidi wachangamkie fursa za kujenga mwendo mbinu za kisasa kama vile kiwanja cha kisasa cha michezo.Malls,Soko kubwa la kisasa,majengo ya kisasa Katikati ya mji ili kuvutia watu kuhamishia makazi yao Morogoro kwani ni mji unaounganisha mikoa ya kusini, magharibi na kaskazini(tokea Handeni,Turiani).Rais wetu anatupa Dira na wana Moro tuchangamkie hizi fursa.
Naheshimu maoni yenu but kwaniniulaumu watanzania wote kwa kosa la mtu au watu wachache. Kwani mmiliki wa uwanja ni nani ? Kwanini nilaumiwe mimi niliyepo musoma wakati kuna wamiliki au wasimamizi wa huo uwanja. Kwanza viwanja vingi Tanzaniavinamilikiwa na ccm chama ambacho mwenyekiti wake ni mtukufu Rais. Pili maswala ya watu sijui akina malinzi, bomba la mafuta mara ndege mi naona yote haya hyahusiani na swala la muanzishaji wa mada labda kama alikuwa na lengo la kuongelea siasa mahali ambapo siyo sahihi. Hayo mengine kama la ndege linahtaji mitazamo tofauti na asidharauliwe yule mwenye mtazamo tofauti na wako coz siyo afya wote kuwa na mtizamo mmoja muda flani
ReplyDeletetatizo lakujiona una akili sana kuliko hata wazee wako mwisho wake huishia katika majuto,endelea kujiweka ktk kundi la great thinkers wakati we ni kilaza namba 1
ReplyDeleteMkuu, inaonekana umekaa nje ya nchi muda mrefu na hujui kinachoendelea nchini kwako. Kwa taarifa yako, viwanja karibu vyote, ukiondoa (Azam Complex) na vina milikiwa na CCM na serikali. Ukumbuke viwanja hivi ni vile ambavyo vingi vilijengwa wakati wa utawala wa chama kimoja. CCM huvitumia viwanja hivyo kufanyia sherehe mbalimbali. Na linapokuja swala la soka wao kazi yao ni kudai malipo kwa matumizi, lakini usiwaambie swala la kuvitunza kabisa. Unajua hilo kama hujui ungeuliza uambiwe. Unapotoa maneno ya shombo huku ukiwa unajua mmiliki hutendi haki kwa watanzania. Kwanza, urudi nyumbani utoe mchango wako katika moja ya vilabu vyetu kujenga viwanja vyao. Hapo tutakuwa tumewaweza CCM kubaki na maviwanja yao wafugie mbuzi.
ReplyDelete