April 7, 2018



Hali ya kikosi cha Majimaji Fc imezidi kuwa mbeye katika Ligi Kuu Bara baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Mwadui FC.

Majimaji ilikuwa ugenini mkoani Shinyanga ikikaribishwa na Mwadui FC na kukubali kichapo cha idadi hiyo ya Mabao.

Mabao ya Mwadui yalifungwa na Paul Nonga kwenye dakika ya 6 na 56, huku jingine lilikifungwa na Miraji Athumani dakika ya 45.

Majimaji walijipatia mabao yao kupitia kwa Marcel Kaheza katika dakika za 64 na 85.

Matokeo yamezidi kuiweka Majimaji pabaya kwenye msimamo wa ligi, sasa wameendelea kujichimbia chini kwa kusalia na alama zake 16.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic