Mkude alitangazwa kushinda nafasi hiyo mapema baada ya mchezo dhidi ya Yanga kumalizika kwenye Uwanja wa Taifa jana ambapo Simba walifanikiwa kushinda kwa bao 1-0.
Mbali na kuchagulia na mashabiki, mchezaji wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua, ameeleza kuwa Mkude ndiye mchezaji bora pia kwake, kutokana na namna ambavyo alicheza jana Uwanjani.
Chambua amesema kuwa Mkude alikuwa akitengeneza mipira mizuri katikati mwa Uwanja na kuwalisha wenzake, huku akishindwa kuipoteza bali aliihimili vizuri.
Chambua amempa nafasi ya ubora Mkude katika mchezo baada ya kuiongoza safu ya kiungo vizuri na kuifanya iwe bora zaidi dhidi ya watani zao Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment