Mshambuliaji wa FC. Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi, amemtakia kheri mchezaji mwenzake Andres Iniesta ambaye jana ametangaza rasmi kustaafu kuichezea soka timu hiyo kutoka Catalunya.
Messi ameeleza kuwa ilikuwa ni faraja kubwa na wakati mzuri kwake kucheza sambamba na Iniesta kwa miaka yote ambayo walikuwa wote Camp Nou.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, Messi amemtakia kheri mchezaji huyo ambaye ameamua rasmi kuachana na Barcelona na kwenda kutafuta maisha yake ya soka mahala pengine.
Iniesta alitangaza jana kuachana na Barcelona akiwa ameichezea kwa miaka 22 baada ya kujiunga nayo mwaka 1996.
Kiungo huyo aliyeng'ara zaidi wakati akicheza na Xavi, amefanikiwa kutwaa mataji 31 sawa na Messi ambaye bado anaichezea Barcelona.
Bado haijajulikana atajiunga na klabu ipi ingawa kumekuwa na taarifa zinazoeleza anaweza akatimkia Manchester City ama kuelekea China.








0 COMMENTS:
Post a Comment