April 28, 2018



Na George Mganga

Kikao cha Bunge kiliendelea jana katika Makao Makuu ya Bunge jijini Dodoma kwa hoja mbalimbali kuendelea kujadiliwa zinahusiana na masuala ya nchi.

Wakati kikao kikielekea mwishoni, Mwenyekiti wa Bunge na Mbunge wa Wilaya ya Ilala, Mussa Azzan Zungu, aliwamchokea swali la kiaina Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dr. Harisson Mwakyembe, kuhusiana na kufungiwa kwa wimbo wa Mwanaume Mashine ulioimbwa na Msanii, Msaga Sumu.

Zungu alimuuliza Mwakyembe kwanini ameufungia wimbo huo wakati umewataja wachezaji Simon Msuva (aliyekuwa anaichezea Yanga) na Shiza Kichuya ilihali timu hizo zinakutana kesho kwenye Uwanja wa Taifa.

Zungu aliwataja wachezaji hao kutoka na namna mchezo huu wa watani wa jadi jinsi unavyovuta hisia za mashabiki na wadau wengi wa soka nchini ambazo zitakuwa zinavaana Jumapili hii ya Aprili 29 2018.

Swali hilo lilipelekea kuwaacha hoi wabunge wengi ambao walianguka kwa kicheki na ndipo Mh. Zungu akafunga kikao na kuwataka wabunge watakutana wakati mwingine kuendelea na vikao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic