April 6, 2018



Na George Mganga

Wakati zikiwa zimesalia siku mbili mbili kuelekea mchezo wa ligi kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Simba Jumatatu ya Aprili 9 2018, Mkude yuko fiti asilimia 100 kucheza mchezo huo.

Kwa mujibu wa Daktari wa timu, Yassin Gembe, amesema tayari Mkude ameshapona na sasa limesalia jukumu la Kocha Pierre Lechantre kuamua kama atamtumia dhidi ya Mtibwa.

Gembe ameeleza kuwa kiungo huyo ameshaimarika vizuri baada ya kuanza mazoezi mepesi siku kadhaa zilizopita kufuatia kupatwa na maumivu ya kifundo cha mguu wake wakati timu ikiwa jijini Dar es Salaam.

"Mkude tayari alishaanza mazoezi muda mrefu, ameshapona kabisa na sasa litakuwa jukumu la kocha kama ataamua kumtumia" amesema Gembe.

Mkude aliumia wakati Simba ikijinoa Uwanja wa Boko Veterani ikiwa katika harakati za maandalizi dhidi ya Njombe Mji FC, baada ya kukwaana na Mzamiru Yassin wiki jana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic