April 9, 2018



Na George Mganga

Kipute kimoja cha mchezo wa ligi kuu bara kinapigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambapo Mtibwa watakuwa wenyeji kuikaribisha Simba.

Timu zote zinakutana zikiwa na kumbukumbu ya kushinda michezo yake ya ligi iliyopita ambapo Mtibwa waliilaza 3-0 Singida United na Simba wakiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Njombe Mji FC.

Mtibwa wametamba kuelekea mchezo huo kuwa hawana hofu na Simba na dozi waliyowapa Singida United wataihamishia Uwanja wa Jamhuri leo.

Kupitia Msemaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru, tayari ameshaweka tambo zake akisema hawana hofu na Mnyama kutokana na kasi waliyokuja nayo.

Mtibwa imeshinda mechi zake mbili mfululizo zilizopita ikiwemo dhidi ya Azam FC kwenye FA na Singida United katika ligi.

Mchezo huo utaanza saa 10 kamili jioni ya leo.

3 COMMENTS:

  1. Mtibwa wnasema hawatishwi na Simba. Kweli yupo asiyemuogopa Simba? Msije mkatokea kwa mlango wa nyuma baada ya kulazwa na mngurumo wa mntama bana

    ReplyDelete
  2. Tulia tuli,tusubirie muda SIMBA hatishiwi kwa maneno yeye ni vitendo tu,watakimbia leo kichuya,boko na okwi wanaua.

    ReplyDelete
  3. Sasa wataniamin,nilisema hapa hii formation sio ya mchezomchezo,KICHUYA+BOCCO+OKWIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic