April 3, 2018



Nahodha wa kikosi cha Singida United, Nizar Khalfan, ametoa onyo kwa wachezaji wa timu yake kutobweteka mapema na ushindi dhidi ya Yanga.

Singida iliiondoa Yanga katika mashindano ya Kombe la Shirikisho kwa changamoto ya mikwaju ya matuta baada ya dakika 90 kumalizika kwa matokeo ya 1-1.

Khalfan amewataka wachezaji wa kikosi hicho kutoridhishwa kuindosha Yanga mapema huku akiwaomba wazidi kupiga moyo konde mpaka wahakikishe wanachukua ubingwa wa FA.

"Ni mapema sana kukata tamaa, wachezaji hawatakiwi kuridhishwa na ushindi dhidi ya Yanga kwa maana mashindano si rahisi, na wote waliofika nusu fainali wamepambana" alisema Niazr.

Singida United ilifika hatua hiyo ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa matuta 4-2 dhidi ya Yanga na kuungana na timu za JKT Tanzania, Stand United na Mtibwa Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic