Beki wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars, Boniface Pawasa, amefunguka kwa kueleza kuwa mechi ya watani jadi kati ya Simba na Yanga haitokuwa rahisi.
Pawasa aliyewahi kung'ara akiwa na Simba, amesema kuwa timu hizo zimekuwa na uwiano sawa wa kupata matokeo katika mechi zake za mwisho za ligi kwa kwenda sare, hivyo lazima mechi iwe ngumu.
Simba na Yanga zilienda sare kwenye michezo yao ya mwisho ya Ligi Kuu ambapo Simba alipata matokeo ya bao 1-1 na Lipuli huku Yanga akipata dhidi ya Mbeya City FC.
Licha ya hilo, Pawasa amesema pia ujio wa Kocha mpya Yanga, Mkongomani Zahera Mwinyi, unaweza ukawaharibia kuelekea mechi hiyo sababu ameeleza yawezekana akaja na falsafa mpya ambayo inaweza ikawa tatizo kwa wachezaji.
"Ujio wa Kocha mpya Yanga unaweza ukawa tatizo kwa maana Mwalimu ni mpya, inawezekana akaja na falsafa mpya ambayo inaweza kutoshikwa kirahisi na wachezaji" alisema Pawasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment