April 6, 2018



Kikosi cha Simba kimemaliza rasmi kambi yake ya muda mfupi iliyoweka mjini Iringa ambapo leo itaanza safari ya kuelekea mjini Morogoro.

Kikosi hicho kilisafiri kutokea mjini Njombe mpaka Iringa Jumatano ya Aprili 4 2018 kuweka kambi maalum ya muda mfupi ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuikabili Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi Jumatatu ya Aprili 9 2018.

Simba itakuwa na kibarua dhidi ya wakata miwa hao ambao leo wanakaribishwa na Singida United kwenye mchezo wa ligi kwenye dimba la Namfua.

Wekundu hao wa Msimbazi wataendelea na mazoezi kesho wakiwa mjini Morogoro huku wakisubiria kibarua chao cha Jumatatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic