Uongozi wa klabu ya Simba umesema unaamini kabisa waamuzi wa mechi yao dhidi ya Yanga Jumapili, watatenda haki.
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema hawatawalalamikia waamuzi kabla lakini wanaamini kikubwa ni haki.
“Waamuzi watakaocheza tunaamini watafuata sheria 17 za soka kwa ajili ya kufanya haki itendeke,” alisema.
Simba inashuka dimbani Jumapili kuivaa Yanga katika mechi ambayo kama watashinda, basi watakuwa wamejihakikishia kubeba ubingwa kwa asilimia 95.
0 COMMENTS:
Post a Comment