April 23, 2018




Mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho 'Azam Sports Federation CUP' unatarajiwa kupigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.

Tayari JKT Tanzania wameshawasili mjini humo wakiwa wamekamilisha maandalizi yao kuelekea pambano hilo litakaloanza saa 10 kamili jioni.

Mshindi wa mechi hiyo ataungana na Mtibwa Sugar FC katika hatua ya fainali itakayopigwa June 2 2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Mtibwa walitinga fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United, katika mchezo uliopigwa mjini Shinyanga kwenye dimba la CCM Kambarage.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic