April 4, 2018




Na George Mganga

Kikosi cha Simba kimewasili salama mjini Iringa ambapo kitaweka kambi maalum ya muda mfupi kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Simba watakuwa wageni dhidi ya Mtibwa Sugar Jumtatu ya wiki ijayo itakayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Vinara hao wa Ligi Kuu Bara wameamua kufanyia maandalizi yao mjini Iringa baada ya kuvuna alama tatu muhimu dhidi ya Njombe Mji FC jana Jumanne na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo mwa Ligi Kuu Bara.



Katika mchezo wa jana Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Nahodha John Bocco.

Baada ya kuwasili mjini Iringa leo, kikosi hicho kitaanza mazoezi kesho tayari kwa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic