Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ pamoja na wajumbe wa kamati ya Utendaji ndiyo waliopambana vilivyo wakati Simba ikiwa nchini Misri.
Wajumbe wa kamati ya utendaji ni Musleh Al Rawah, Said Tulli pamoja na rafiki wa Simba aitwaye, Mathew.
Taarifa zinasema wakiwa Morogoro waliendelea na kazi yao ya kuwahamisha wachezaji na pia kuhakikisha kila kitu kinakwenda sahihi.
“Kweli wanajitahidi sana na wachezaji wanajisikia vizuri kwa kuwa ni watu ambao wanafanya kazi yao kwa kujituma,” alieleza mdau aliyezungumza na SALEHJEMBE.
“Unajua wachezaji wako katika hali nzuri, wako vizuri kisaikolojia kwa kuwa kila kitu kinakwenda kwenye msitari na jamaa wanataka kuona suala la wachezaji linabaki uwanjani wao kucheza, wakiwa hawana malalamiko.”
Wakati wakiingia kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, kulianzisha gumzo, wengi wakiwajadili na kusema kama wao wanaingia, basi Mtibwa wajue safari inawakuta.
Nimoja ya kazi yao
ReplyDelete