Presha ya mchezo inaweza kukufanya ukafanya maamuzi ambayo ni magumu, ndivyo ilivyokuwa baada ya nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani kuonekana akizuia mabadiliko ya kumtoa kiungo, Papy Tshishimbi katika mchezo wa jana dhidi ya Simba.
Tukio hilo lilitokea kipindi cha pili baada ya Simba kuwa mbele kwa bao 1-0 huku Yanga wakiwa pungufu kutokana na beki Hassan Kessy kupewa kadi nyekundu, ndipo benchi la ufundi likawa linataka kumtoa Tshishimbi lakini Yondani akaelekea kwenye benchi na kuonekana akitoa ushauri wa kutofanya hivyo.
Licha ya ushauri huo bado Tshishimbi alitolewa katika dakika ya 80 na nafasi yake kuchukuliwa na Emmanuel Martin lakini hiyo haikuchangia kubadilisha matokeo ya mchezo huo ambapo Simba ilishinda bao 1-0.
CHANZO: CHAMPIONI
Nilifurahishwa sana na mpira wa Yanga dakika 15 za mwanzo.maana hata Simba wenyewe waliamini wanakufa.lkn baada ya hapo Yanga waliingia ktk mtego wa Simba wakaiga mpira wao.hilo ni kosa.hata hivyo mpira ni ujanja,mbinu na ufundi.hayo ndiyo maeneo ya nguzo za ushindi mpirani.mzungu wa Simba aliwajua Yanga kuwa nguvu zao zote watawekeza katika kumbana Okwi,Chiza,na Bocco Hram.Hivyo alitumia mbinu ya kumwekeza yule mfungaji atumike kama mfungaji mbadala wa siku ya jana.na nilimwabgalia sana mzungu yule full time yuko wima anakiendesha kikosi uwanjani kama kwa remote control kama atakavyo yeye,wakati huo wote benchi la Yanga wamepigiliwa misumari kwenye fomu.
ReplyDeleteHabari ya kumtoa Ajib na Tshimbi kwa nyakati kama zile ni sawa na kufumua kenchi nyumba wakati wa mvua kali.hata hivyo si angeinguzwa j.Abdul na Ninja basi!!!?
Ahaa!yametokea.ujue Yanga walikuja kutuliza dakika 10 za mwishoni,hapo niliuona tena ule mpira wao ea mwanzoni walioupoteza lkn haikusaidia ni kama kukumbuka shuka kumekucha.
Nawapongeza sana deffence ya Yanga iliyoongozwa na Yondan,imefanya kazi kuvwa.Mjue Simba walileta kikosi cha kawaida tu,wachezaji walewale isipokuwa ufundi,ujanja wa porini na mbinu ndizo zilizo wazalia gili lile moja.Yanga tengenezeni kikosi sakeni washambuluaji wapya na middle fielders aa kutosha kabla hamhasonga mbele.Wekezeni kwenye hilo,maana mpira ni biashara siku hizo mbali ya kywa ni burudani pia.Ni biashara.tafuteni wafanyakazi bora wa biasgara yenu jama mnataka kusonga mbele Acheni manenomaneno ya kywajaza mashabiki uongo na mbwembwe,ohoi kamusoko ndani,oho Mboma na Tambwe hawajambi watakywepo.Hiyi mbwembwe gaziwasaiidii kwenye biasgara ya mpira.wekeni dau ingizeni wachezaji wenye kusukuma biashara ya mpira.yuko wapi yule deffender mzaire? Kimyaaa! Maneno maneno kwenye biashara hii hayatakiwinia ni kuwekeza wachezaji tusonge mbele club ipate pesa maebdeleo yaonekabe.mnaingiza timu kucheza mashindano ya kwa mataifa kanakwamvwa timu inaenda kucheza na Tazara biys jamani? Hao mnaowafuata ambao mumepangiwa kwenye kundi moja,wamewekeza wanazitamani pesa zile.Mpura ni biashara.mubadilike.msibaki oho kikosi cha bilioni moja bilioni moja wimbo huo ufutwe akilini.fanyeni harambee mnaelejea segemu kubwa ya uchezaji inahitaji uwekezaji mkubwa.