Na George Mganga
Kocha Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga. Hata hivyo, bado kuna hali ya sintofahamu.
Hali hiyo inatokana na ile kauli ya Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa kusema kwamba bado wanamuangalia Zahera na hawajampa mkataba.
Lakini baadaye kumekuwa na picha inazunguka mitandaoni na taarifa zinaeleza, Mkongo huyo amesaini miaka miwili.
"Sasa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DRC, kweli anaweza akaangaliwa Yanga. Jamani hata nyie angalieni hapo, amesaini mkataba tayari labda kuwe na jambo jingine au kocha kaona amekosea, kaamua kuondoka," kilieleza moja ya chanzo.
Zahera amechukua rasmi mikoba ya Mzambia aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha Yanga baada ya kuondoka kimyakimya kurejea kwao Zambia katika klabu yake ya zamani, Zesco United.
Zahera alichelewa kusaini mkataba na Yanga kutokana na majadiliano baina yake na uongozi wa klabu hiyo, lakini sasa wamefikia mwafaka na ameamua kuweka kandarasi hiyo itakayomalizika mwaka 2020.
BADOOOOO HAUJASEMA, WAAMBIE WASOMAJI WAKO ATA ARAFAT DJAKO NAYE AMESHASAINI LEO
ReplyDeleteNafikiri tusubiri majibu yatapatikana haina haja ya kufosi mpira unachezwa sehemu ya wazi yote yatakua bayana.hakuna kadi ya mwaliko kwenye fumanizi
ReplyDeleteMwandishi unauliza maswali tena? Njoo na jibu , kuna tatizo gani! Kocha kuangaliwa? Mambo ni mengi ktk soka.
ReplyDeleteTena hukupaswa kushangaa hilo kama umebaini ni kocha bora kwa CV Aliyonayo Yanga haitakiwi kukurupuka.
Mwandishi unauliza maswali tena? Njoo na jibu , kuna tatizo gani! Kocha kuangaliwa? Mambo ni mengi ktk soka.
ReplyDeleteTena hukupaswa kushangaa hilo kama umebaini ni kocha bora kwa CV Aliyonayo Yanga haitakiwi kukurupuka.