May 19, 2018


Mahamaka Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imekubali maombi ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Michael Richard Wambura ya kufanya marejeo dhidi ya maamuzi ya Kamati za shirikisho hilo.

Hukumu kwenye shauri hilo namba 20/2018 imetolewa leo na Jaji Wilfred Ndyasobera baada ya kuridhika na hoja zilizotolewa na mawakili wa Wambura, Dk. Masumbuko Lamwai na Emmanuel Muga.

Maamuzi hayo yanatokana na maombi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu wiki mbili zilizopita yakiomba Mahakama imruhusu Wambura afungue kesi ya msingi kuomba kutengua maamuzi ya Kamati za TFF.


Mahakama imetamka kuwa Wambura ana kesi yenye misingi mizito na ambayo inafaa isikilizwe na Mahakama; kwa Kiingereza alisema: ‘Wambura has fit case for further consideration by this court”.

Muga amesema kwamba Mahakama imeridhika kuwa maombi yaliletwa ndani ya muda, na Wambura ana maslahi mapana ya kuleta maombi, hivyo mahakama imempa ruksa ya kuleta kesi ya msingi ya kuomba kutenguliwa kwa maamuzi ya kamati za TFF.




Amesema Mahakama imeamuru kuwa kesi ya msingi ifunguliwe ndani ya siku 14 kuanzia leo, kwa hiyo kesi hiyo itafunguliwa kama mahakama ilivyoagiza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic