May 18, 2018




Na Saleh Ally
YANGA imekwama, si vibaya kusema imekwama katika tope na inaonekana ni kama vigumu sana kukomboka na kuingia katika barabara sahihi.


Yanga haiende kwa mwendo wake, ajabu zaidi inaonekana kama mambo yanakwenda haraka sana na zaidi ni kudidimia.

Mashabiki wengi wa Yanga wamekuwa ni watu wenye jazba na wanahizi kila mtu ni msaliti kwao, sasa hawataki hata kuona timu au klabu yao inatajwa.


Siku chache zilizopita, walitamani Yanga itajwe, walitamani kuiona inazungumziwa na ikiwezekana kupewa heshima kubwa kutokana na kile unachokifanya.

Lakini sasa mambo yamekuwa tofauti, ikizungumzwa Yanga ni ukata ndicho kinachosikika sana kwa kuwa imekuwa ni timu yenye maisha mazuri kwa muda mrefu, tokea mwaka 2012.


Kama unakumbuka, baada ya Simba kuifunga Yanga kwa mabao 5-0 na kubeba ubingwa, maumivu ya Wanayanga yalikuwa ya kiwango cha juu. Ndipo aliyekuwa mfadhili alipoamua kugombea uenyekiti.

Yusuf Manji aliamua kugombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu hiyo akisisitiza kwamba klabu hiyo ilihitaji mtu imara ambaye angeweza kusimama imara na kurejesha umoja wa Wanayanga ambao walikuwa wamesambaratika baada ya kipigo kile kikali kutoka kwa watani wao.


Kwa muda aliokaa madarakani, Manji alifanikiwa kwa asilimia mia. Aliiwezesha Yanga kuwa bingwa mara nne katika misimu mitatu, ikifanikiwa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho hatua ya makundi. Kama hiyo haitoshi, aliiwezesha Yanga kuibana Simba kushindwa kushiriki michuano ya kimataifa kwa muda wote huo.

Manji aliibana Simba kwa kuwa Yanga ilikuwa ikichulkua nafasi hiyo na kufuatia na Azam FC. Simba ikazorota na machungu yakahamia Msimbazi ambao walikuwa wakipambana kwa kila namna kurejesha heshima yao.


Kwa Yanga sasa wametumbukia katika shimo ambalo walikuwemo Simba ambao wanaonekana wamepindua kabati na huenda wako wanaona hali hiyo inaweza ikawa ni ya siku mbili au tatu, hilo ni kosa kubwa sana.


Hali inayowatokea Yanga katika kipindi hiki haiwezi kwisha wka ramli au miujiza. Na Kama Yanga wataendelea kuamini itaisha tu kwa kudra zake muumba, basi wataendelea kutesekwa kipindi kirefu sana.


Yanga hawajaingia katika shimo hilo kwa bahati mbaya. Badala yake, suala hilo lilikuwa linakua hatua kwa hatua huku ikionekana kama ni suala ambalo haliwezi kutokea.


Mwisho limetokea na kuwa mzigo mzito kwa Yanga ambayo sasa haitakiwi kufanya kazi kwa hisia pekee, badala yake uteketezaji wa vitendo unatakiwa kwa zaidi ya asilimia mia.


Wengi wa viongozi au wadau wa Yanga ni wale waliokuwa wakipiga kelele kama akina Salum Mkemi na wajumbe wenzao kuonyesha kwamba wana mipango imara sana ambayo sasa haionekani wakati Yanga ikididimia.


Watu kama hao, wakiwemo kama Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, sasa wameanza kuona mziki ni mkubwa na utaona wamekuwa kimya hakuna anayezungumza tena kama ilivyokuwa katika kipindi cha Manji. Kwamba anajinufaisha na klabu. Sasa hayupo na mambo ni magumu.

Yanga inaweza kujikomboa na kujitoa kwenye tope na ndilo jambo linalotakiwa kufanyika. Lakini lazima ipate kiongozi ambaye atakuwa ndiye mkuu, akubali lawama zote ili kufanya mabadiliko.

Yanga inapaswa kupata mtu aliyenuia kuing’oa ilipo, lakini lazima awe mtu asiyebabaishwa na maneno au zile lawama ziliokuwa zikitolewa kama wakati ule wa Manji.


Kuikomboa Yanga lazima awe mtu mwenye ndoto ya mafanikio ya kibiashara, mtu anayeangalia kinachoingia na kinachotoka na mwenye mipango ya muda mrefu na mfupi.

Lazima mtu huyo awe ni mwenye mapenzi ya dhati na Yanga, asiyetaka kujifaidisha binafsi kwa kuwa Yanga imeathirika kwa kiasi kikubwa na watu wengi waliotaka kujifaidisha wao na nafasi zao na  si klabu.


Naweka msisitizo, Yanga inahitaji mtu mkweli asiye mwoga, mwenye mipango sahihi ya biashara na uzoefu wa uongozi ambaye atarekebisha ilipofikia, la sivyo itajikuta katika mateso ya muda mrefu sana.


Kwa mashabiki na wanachama wa Yanga, punguzeni lawama. Kuweni mnaowapa moyo wanaojaribu kufanya vizuri kwa ajili ya klabu yenu. Kama mtaendelea hivyo, basi hata wenye uwezo watawakimbia kwa hofu ya lawama zisiosha.


5 COMMENTS:

  1. Hii makala nyingine bora kabisa na yenye kila aina ya uweredi. Nakupongezeni saleh jembe...

    kiukweli katika soka la nchi hii kuna mambo ambayo mtu mwenye utimamu hawezi kutuelewa na ndio maana kila siku tupo pale pale .. mpira wa leo morden football its all abt investment,to run a football club its a science now days. Nakuelewa sana kuhusu watu kama mkeni na yule mzee anaendeshwa na njaa ya tumboni kwake. Mpira wa leo hauwahitaji watu kama mkemi wala akili mali,mpira unahitaji wataalamu na sio wanachama tuu bila weredi,kama mtu hana utaalamu bas abakie kuwa mwanachama wa kawaida tu pia si vibaya. Nataman kila mwana yang asome makala hii na ile nyingie ya WALIOMPINGA MANJI WAKO WAPI????... hii ni kipimo sahihi kujua nani anatufaa na nani hafai pale yanga hata kupewa kazi ya kufagia. Bro dont get tired to write and help our football to prosper. Kazi nzuri

    ReplyDelete
  2. Tabu yenyewe yanga inategemea waganga wakienyeji kuondoa matatizo na kupata mafanikio na huku heala yao ikiliwa hovyo.Sasa mambo yamefika ukingoni na Manji kajitoa na wala hataki,kusikia lolote. Fika kutani na pesa yote poteya na kila kitu iko haribika na mimi hapana heshima tena. Sitaki ona jumbe yoyo jumbani yangu

    ReplyDelete
  3. Hapo sijaelewa, "imechukua ubingwa mara nne katika misimu mitatu"

    ReplyDelete
  4. Najivunia kuwa na mtu mweledi na asiye simama upande wowote ndio maana hata kabla sija amka lazima nipite kwenye ukurasa wake sio blog zingine zenye mihemuko na chuki.

    ReplyDelete
  5. Moja kati ya makala bora kabisa kwangu hii naiita makalatiba,ukweli ni kwamba wanayanga tumejiroga wenyewe hatupaswi kumtafuta mchawi nje mchawi yupo ndani ya yanga....wakati Manji alipoamua kuomba dhamana ya wanachama ili akabidhiwe timu wengi wetu tulikubaliana na hili suala lakini kwa maakusudi baadhi ya watu ambao kwa kulinda maslahi yao binafsi na wengine wakiwa viongozi tuliowapa dhamana ya kutuongoza,walikuja na maneno matamu yenye kuleta faraja na ushawishi mkubwa mpaka ikafikia hatua ya kumuona Manji kama ni mtu asiye na manufaa na mwenye lengo la kutaka kujinufaisha binafsi,leo hao ambao walitufanya wanayanga tuamini mabadiliko ya uendeshaji hayana tija wamekimbia na hakuna hata mmoja ambaye amethubutu kusimama na kutupa dira mpya....wanayanga huu ni wakati wa kusimama na kufanya maamuzi magumu ili kuinusuru club yetu ambayo kila kukicha inazidi kuzama kwenye tope.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic