DANY LYANGA AREJEA KAZINI
Baada ya kumrejesha Mzimbambwe, Elisha Muroiwa, Singida United imezidi kurejesha dhana zake ambapo mchezaji Dany Lyanga naye amerejea kikosini kufuatia kukwamishwa na sakasaka la usajili wake.
Lyanga alishindwa kukichezea kikosi hicho kutokana na usajili wake kushindwa kukamilika wakati anatokea Fanja SC ya Oman.
Mshambuliaji huyo hakuweza kuwa na kikosi baada ya usajili wake wakati wa dirisha dogo kushindwa kufanikiwa hivyo kwa sasa ataendelea na mazoezi mpaka pale dirisha jipya la usajili litakapofunguliwa utakamilika.
Hapo awali taarifa ziliezwa kuwa Lyanga alifungikwa na FIFA kutokana na kusaini mkataba zaidi ya mmoja kati ya Fanja na Singida United.
Sasa kifungo kimeisha?
ReplyDeleteKifungo bado hakijaisha hapo.
ReplyDeleteSingida nao suala la usajili wapo tu km timu ya wananchi
ReplyDelete