May 16, 2018


Timu anayoichezea Mtanzania Simon Msuva imekubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya TP MAzembe katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Stade El Jadid usiku wa Jumanne.

Katika mchezo huo ambao ni wa kundi B, Jadidi walionekana kuawala kwa asilimia kubwa lakini dakika 45 za kwanza zikimalizika kwa milango kutofungika.

Jadid ambao walikuwa nyumbani walianza kufungwa bao la kwanza kupitia kwa Malango mnamo dakika ya 51 na dakika tano baadaye, Sissoko akaongeza la pili kwenye dakika ya 55.

Mpaka dakika 90 za mchezo huo zinamalizika, Jadid walikuwa nyuma kwa mabo 2-0.

Matokeo hayo sasa yanailazimu Jadid kushinda mechi ya marejeano kuanzia mabao matatu kwenda mbele bila nyavu zao kuguswa ili kujitengeneza mazingira mazuri ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic