Ndugu Leodegar Chilla Tenga, Mwenyekiti Baraza la Michezo la Taifa, Wajumbe wa Baraza la Michezo la Taifa,
Viongozi wa Mashirikisho/Vyama Kitaifa,
Watumishi wa Baraza la Michezo la Taifa,
Viongozi wa Mashirikisho/Vyama Kitaifa,
Watumishi wa Baraza la Michezo la Taifa,
Wanahabari,
Mabibi na Mabwana.
Mabibi na Mabwana.
Habari za Asubuhi.
Awali ya yote ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujalia uzima na kutuwezesha kuwepo mahali hapa siku hii ya leo.
Ndugu Mwenyekiti, kwanza napenda kukupongeza wewe binafsi pamoja na Wajumbe wote mlioteuliwa kuunda BARAZA hili la kumi na nne. Vilevile ninampongeza kwa dhati Mwenyekiti na Wajumbe wote waliokuwa katika Baraza la kumi na tatu.
Ndugu Mwenyekiti, ni imani yangu kuwa tumefanya uteuzi wa Wajumbe wa Baraza la Michezo kwa kuzingatia umakini na uwezo wenu kwa kila mmoja tukiwa na malengo ya kuongeza ufanisi wa chombo hiki muhimu katika usimamizi wa Maendeleo ya Michezo nchini. Mmeteuliwa ili kuleta mabadiliko makubwa katika Sekta ya Maendeleo ya Michezo.
Kazi kubwa mnayokwenda kuifanya imefafanuliwa vyema katika Sheria inayounda Baraza la Michezo la Taifa, ambayo ni Sheria ya Bunge Na. 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake Namba 6 ya mwaka 1971. Sheria hii
1
imeainisha vema kazi na wajibu wa BARAZA katika kuendeleza michezo hapa nchini.
Ndugu Mwenyekiti, pamoja na kazi za Baraza la Michezo la Taifa zilizoanishwa kwa mujibu wa Sheria, Baraza hili litapewa majukumu ya ziada au ya nyongeza kutokana na hali halisi ya michezo ilivyo kwa sasa hapa nchini. Nyongeza hii, itatokana na ukongwe wa Sheria yenyewe, hali inayosababisha baadhi ya kazi kushindwa kutekelezeka kama inavyotarajiwa hivyo yanahitajika maelekezo ya ziada.
Ndugu Mwenyekiti, Kazi za nyongeza ambazo zinahitaji utekelezaji wa haraka ni pamoja na:-
- Kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo nchini ambao utakuwa na vyanzo endelevu vya mapato. Ili kufanikisha jambo hili lazima vyanzo vya mapato vya kisheria VIBORESHWE na vyanzo vipya vibuniwe na kuanzishwa ili kumudu majukumu mapana ya BARAZA.
- Kwa mfano, moja ya chanzo cha mapato ya BARAZA ni asilimia kumi (10%) ya bei ya kiingilio ya tiketi katika michezo yenye viingilio. Hili halijawahi kutekelezwa na BARAZA. Vilevile, ukusanywaji wa maduhuli kutoka katika Michezo ya Bahati Nasibu ya Taifa haufuatiliwi.
- Kuendelea kufanya Mapitio ya Sheria iliyounda BARAZA ili kuwa na Sheria inayoendana na hali halisi pamoja na matakwa ya Maendeleo ya Michezo ya leo Tanzania na Duniani kote.
- Chini ya Uongozi wako pamoja na timu uliyonayo hakikisheni mnafanya Mikutano na Wadau wa Michezo katika ngazi za Mikoa na
2
Wilaya kubaini changamoto zao na kufuatilia maendeleo yao. Hivi sasa Mikoa na Halmashauri zote zimejitahidi kuajiri Maafisa Michezo, ambapo kazi yao ni kusimamia na kuhamasisha michezo katika ngazi hizo za Mikoa na Wilaya. Iwapo kutakuwa na mipango endelevu ya Maendeleo ya Michezo katika ngazi ya Taifa (BARAZA) hadi Wilaya ambako ndiko chimbuko la vipaji vya michezo na mipango hiyo ikisimamiwa vilivyo kwa ushirikiano baina ya BMT, Mikoa na Wilaya, ni dhahiri tutapata maendeleo mazuri katika Sekta ya Michezo. Ili kufanikiwa katika jambo hili, ninaliagiza Baraza lako kuhakikisha kuwa linaongeza ushirikiano kwa kupitia Vikao na Mikutano yenye tija kwa Mikoa na Wilaya zote.
- Kutoa mafunzo ya Utawala bora na namna nzuri ya kuongoza Vyama na Mashirikisho ya Kitaifa ili kupunguza changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro isiyo ya lazima na kuleta ustawi katika kuendeleza michezo nchini.
- Nina matarajio makubwa chini ya uongozi wako, kwamba kwa mara ya kwanza BARAZA litatekeleza matakwa ya Sheria ya kuandaa tarifa kila mwaka za utendaji na shughuli za BARAZA ambazo, kwa mujibu wa Sheria, zikiwasilishwa kwangu, na mimi naziwasilisha Bungeni.
- BARAZA lihakikishe kuwa vyama vya michezo vinaheshimu Katiba zao kwa kuheshimu VIPINDI VYA UONGOZI na KUFANYA UCHAGUZI muda unapofika. Tuhakikishe kuwa viongozi hawabinafsishi vyama wanavyoviongoza na hivyo kuwavunja moyo wanachama wao. Natuhakikishe kuwa viongozi wa vyama vya michezo (Mwenyekiti,
3
Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Waweka Hazina hawashiki nafas iza uongozi zaidi ya MOJA kwenye vyama tofauti katika aina moja ya mchezo.
Ndugu Mwenyekiti, naweza kuendelea kuagiza utekelezwaji wa kazi nyingine nyingi, lakini naamini hizi chache pamoja na zile zilizopo katika Sheria ya BMT zikitekelezwa vizuri, Maendeleo ya Michezo hayawezi kuwa ndoto ya mbali sana. Vile vile, niwaombe mtumie fursa hii kumchagua Makamu Mwenyekiti ambaye Mwenyekiti asipokuwepo, hamtajisikia kupwaya sana na kuyumba!
Mwisho kabisa, nitumie fursa hii kuwashukuru Wajumbe kwa kukubali Uteuzi. Aidha, mimi pamoja na watendaji wa Wizara yangu tunaahidi kuwapa ushirikiano wakati wote mtakapokuwa mnatekeleza majukumu yenu. Ninawatakieni kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yenu.
Hivyo, napenda sasa kutamka kwamba Baraza la Michezo la Taifa la Kumi na Nne limezinduliwa rasmi!
Ahsante kwa kunisikiliza.
0 COMMENTS:
Post a Comment