May 3, 2018



Taarifa zinaelezwa kuwa Mromania wa Azam FC, Aristică Cioabă, ameondoka chini kurejea kwao baada ya maendeleo dhidi ya kikosi hicho kuwa mabaya msimu huu.

Cioabă amerejea kwao Romania huku Azam ikiwa inajiandaa kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Jumamosi ya wiki hii.

Kocha huyo ameamua kuondoka mwenyewe baada ya taarifa za awali kuripotiwa kuwa ataondoshwa kuitumikia Azam kutokana na uongozi kueleza kuwa kiwango chake kimefikia mwisho baada ya kuendeleza matokeo yasiyoridhisha.

Kocha Msaidizi, Idd Cheche, ndiye amebakia na kikosi hicho ambacho kimebakiza mechi nne pekee kumaliza ligi ya msimu huu.

Kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm ndiye anapewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Mromania huyo ambapo inaelezwa tayari Azam wameshamalizana naye.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic