May 13, 2018



Meneja wa kikosi cha Yanga Hafidh Saleh, amezungumzia kwa ufupi kama kutakuwa na mabadiliko katika kikosi kitakachocheza dhidi ya Mtibwa Sugar leo.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Yanga kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya kwa kufungwa mabao 2-0 kutokana na kutumia kilicho dhaifu.

Saleh ameeleza kuwa yeye kama Meneja na sehemu nyingine ya benchi la ufundi wameshakamilisha majukumu yao kuelekea mechi hiyo, suala la kubadili kikosi wanamwachia kocha wao.

"Suala la kubadilika kwa kikosi si langu, Mwalimu ndiyo ataamua kama anaweza akawaongeza wengine dhidi ya Mtibwa kwasababu mimi sina majukumu ya kufanya hivyo" alisema Saleh.



2 COMMENTS:

  1. Tunaitakia yanga kila la kheri kwa mechi zao za nje

    ReplyDelete
  2. Watapigwa tu hawana timu ya kushindana msimu huu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic