May 13, 2018



Kikosi cha Mtibwa Sugar kinaikaribisha Yanga katika Uwanja wake wa nyumbani, Jamhuri Stadium leo Jumapili kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kuelekea mchezo huo, Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa wamejiandaa kupeleka maumivu kwa wanajangwani amabao tayari wameshaukosa ubingwa.

Kifaru ameeleza kuwa maandalizi yao yapo vizuri huku akijinadi kwa kutamba kama Yanga wakikaza zaidi basi watafungwa bao nne.

Taarifa zinaeleza kuwa hali za wachezaji na morali kuelekea mtanange huo ziko vizuri na wapo tayari kuzitumikia dakika 90.

2 COMMENTS:

  1. Jamani maumivu waliyokwisha kupata yanga yanatosha, yepi hayo mengine mtakayotaka kuwapa?

    ReplyDelete
  2. Kidodomo kilizidi. Pata picha ingekuwa ni Simba imekwenda na wachezaji wawili wa ziada huko Mbeya.Media ingekuwa haziandiki chochote zaidi ingetiliwa mkizi lakini Yanga kimyaa.Kuna mwandishi kaanza kuwadanganya och utajiri unanukia Kagame kwa milioni 250 wakati mishahara ya wachezaji ni milioni 115 bila gharama zingine .Ni wazi sasa mapato na matumizi yaangaliwe. Kuna figisu au uongozi mpya katika kudhibiti mapato.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic