May 30, 2018


Na George Mganga

Wakati dirisha la usajili kwa timu za Tanzania likitarajiwa kufunguliwa siku chache zijazo, Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amezishauri klabu za Tanzania kusajili wachezaji wenye kariba ya Emmanuel Okwi.


Rage ametoa ushauri huo kwa timu zinazotaka kufanya usajili ili kupata wachezaji watakaoweza kuzisaidia klabu kusonga mbele kwa namna moja ama nyingine.

Mwenyekiti huyo wa zamani amemtumia Okwi ambaye anaitumikia Simba kama mfano kutokana na ubora wake ambao amekuwa akiuonesha tangu ajiunge na mabingwa hao wa ligi katika msimu wa 2017/18.

Rage ameeleza kuwa timu za Tanzania zimekuwa zikishindwa kuthamini vipaji vya ndani na badala yake zimekuwa zikisajili baadhi ya wachezaji wa kimataifa ambao wanakosa ubora unaotakiwa.

Kauli hii ya Rage imekuja mapema kutokana na ligi msimu huu kumalizika huku dirisha la usajili likitarajiwa kufunguliwa msimu hivi karibuni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic