May 1, 2018



Kufuatia vikosi vya timu za taifa za vijana chini ya miaka 20 na 17, Serengeti Boys na Ngrongoro Heroes, Kocha wa zamani wa Simba na Dodoma FC kwa sasa, Jamhuri Kihwelo 'Julio', ameshauri Tanzania inabidi iachane na Taifa Stars.

Akizungumza kupitia kipindi cha Spoti Leo 'Radio One', Julio ameeleza kuwa nguzu nyingi zimekuwa zikitumika kwa ajili ya Taifa stars lakini hakuna mafanikio yoyote yanayoonekana.

Julio amesema ni vema sasa nguvu hizo zilizokuwa zinapewa kwa Stars zikahamishiwa kwa timu za vijana ambazo zinaonekana kufanya vizuri kisoka.

Aidha Julio ameshauri ifikie hatua sasa Serikali iachane na Taifa Stars na badala yake zisalie timu za vijana pekee ili zipewe motisha za kuendelea kufanya vizuri kuliko Taifa Stars ambayo imekuwa haina manufaa kwa soka la Tanzania.

Usiku wa kuamkia leo kikosi cha Serengeti Boys kimewasili nchini baada ya kutwaa taji la Mashindano ya timu za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Somalia.

2 COMMENTS:

  1. M/Mungu amemuonya binaadamu kutofanaya kosa moja la hovyo la sababu za msingi la kuumbwa kama binaadamu nalo ni kukimbia na kukata tamaa wakati mtu anapokabikibiliwa na mtihani na badala yake ametakiwa kusimama imara na kukabiliana na mtihani na kuutafutia ufumbuzi. M/Mungu amemlaani mwenye kukata tamaa hata kama mtu huyo yupo katika mazingira ya uhitimisho wa maisha yake hapa duniani. Mawazo ya Julio ni ya kukata tamaa baada ya kupambana kutafuta ufumbuzi wa tatizo. Kwa mfano hawa Serengeti boys watakapofika kuliwakilisha Taifa kama Taifa stars na wakaja kushindwa kuipatia taifa ushindi itakuwaje? Kwanza tatizo la taifa stars sio la wachezaji, tatizo lipo katika bench la ufundi. Timu ya Taifa haijawa kuwa na kocha wa sifa stahiki kwa miaka mingi sasa. Makocha wengi wanaoajiriwa kwa ajili ya taifa stars ni wa majaribio.
    Mfano mdogo kabisa wa kujifunza kutoka kwa simba. Walisajili vizuri na mwanzoni walijiamini kuwa kila kitu kipo sawa lakini wakajikuta bado wanaendelea nakuwa na timu isioaminika. Ndipo viongozi wao walipoamua kubadilisha rubani angani lilikuwa jaribio la hatari lakini ilibidi ili kukabiliana na mtihani na kuushinda na kwa kweli imewalipa. Kukimbia matatizo kamwe sio suluhisho la matatizo bali ni kuzalisha matatizo mengine.

    ReplyDelete
  2. hao ndio watu wanaojiita wadau wanatoa mawazo pumba kama hayo sasa hivi timu ya taifa siyo mbaya kwa hiyo kina msuva, Sammata tusiwaite timu ya traifa kisa timu za vijana zinafanya vizuri

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic