Taarifa za uhakika za wazi kabisa kutoka ndani ya Klabu ya Yanga zinadai kuwa beki wao kisiki Andrew Vicent ‘Dante’, mkataba wake umemalizika rasmi juzi Jumatatu baada ya mchezo wao na Azam FC, hivyo yuko huru kucheza timu yoyote itakayoweza kummwagia fedha.
Msimu huu uliofikia tamati juzi Jumatatu Dante alionekana kuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi cha Yanga tofauti na msimu wa kwanza alipojiunga na timu hiyo pamoja na kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Dante amesema, kwa sasa yuko huru kufuatia mkataba wake huo kumalizika na kwamba, hadi sasa hajazungumzia suala lolote la kuongeza mkataba na Yanga.
“Nipo huru tangu Jumatatu ligi ilipofikia mwisho na mkataba wangu nao ulifikia mwisho, hivyo hadi sasa sijaongea na yeyote kuhusu kuongeza mkataba mpya zaidi nangojea kama uongozi utasema lolote ili niweze kumalizana nao japo kuna dili zangu nyingine ambazo nazisikilizia,” alisema Dante.
ekuwa kama vile yanga sasa wanawakumbusha wachezaji wao kuwa mikataba yao imekwisha. Inaonesha kama vile imekata tamaa jinsi kinyanganyiro kilichokuwepo cha kuwachomoa yanga nyota wao na wasijue la kufanya na kuamuwa potelea mbali liwe litalokuwa. Inatia huruma sana kama tajiri aliyefilisiwa mpaka nyumba anayokaa
ReplyDeletehivi wewe kila siku YANGA huna timu nyingine unayojua wachezaji wao wamemakiza mikataba? wewe kila siku kutoa habari za wachezaji wa YANGA waliomaliza mikataba. acha ujinga huo,timu Tanzania ziko ngapi mpaka uiandame YANGA pekee. nini dhumuni lako
ReplyDeleteacha kasumba dogo..mbona yanga wote mna akili za akili mali, hapo kitu gani kinachokuumiza na wakati jamaa katimiza wajibu wake wa habari.
Deletehahahaha
Delete