May 29, 2018


Wakati Liverpool ikikamilisha dili la usajili wa Mbrazili Fabinho kutoka AS Monaco, inaelezwa Arsenal walikuwa pia kwenye mchakato wa kupata saini yake.

Licha ya Arsenal kuwa na mipango hiyo, Fabinho mwenyewe alikuwa anatamani kuungana na kocha Mspain, Unai Emery aliyetua klabuni hapo kuchukua nafasi ya Wenger.

Vyanzo mbalmbali vya soka kutoka Ulaya vinaeleza Fabinho alikuwa na matamanio ya kucheza soka lake kwenye dimba la Emirates ili kuungana na kocha huyo ambaye ataingoza Arsenal kwenye ligi msimu ujao.

Dili hilo limeenda tofauti baada ya Liverpool kumuwahi kumnyakua kiungi huyo anayekipiga katika timu ya taifa ya Brazil kwa kitita cha paundi milioni 44.

Usajili huo ni moja ya maboresho ya kikosi cha Liverpool ambayo imeanza kuyaboresha huku ikitajwa pia kumuwania kipa wa Allison kutoka Monaco.

2 COMMENTS:

  1. Monaco ya Italy daaaa kaz ipo

    ReplyDelete
  2. Kitendo cha Kukosea kuwa Monaco ni ya Italy kinadhihirisha uongo wako

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic