Baada ya Yanga kutoa suluhu dhidi ya Rayon Sports katika mchezo wa hatua ya makundi wa Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Pierre Lechantre, amefunguka kuwa kitendo cha Yanga kutoa sare nyumbani ni wazi bado wana kibarua kizito kwenye michuano hiyo.
Yanga, juzi ilicheza na Rayon baada ya awali kuchapwa kwa mabao 4-0 na U.S.M Alger ya Algeria, Yanga sasa inaendelea kuburuza mkia kwenye Kundi D.
Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Lechantre alisema kuwa kupata matokeo ya sare katika kiwanja cha nyumbani ni dalili mbaya sababu wapinzani hawatakuwa tayari kupoteza.
“Sikuwepo uwanjani jana (juzi) lakini kwa matokeo ambayo walipata siyo ishara nzuri kwao sababu kutoa sare nyumbani wasitegemee kwamba wataenda kushinda ugenini ni jambo gumu mara nyingi matokeo yanaanza kutengenezwa nyumbani.
“Wasikate tamaa waendelee kupambana ila watambue kwamba wanatakiwa kujituma zaidi uwanjani hasa wanapokuwa nyumbani,” alisema Lechantre, kocha ambaye amefanikiwa kusimamia mechi 14 bila kupoteza tangu atue Simba msimu huu.
Asante kwa ushauri mzee baba
ReplyDelete