MGHANA WA AZAM FC AVUNJA MKATABA WA KUITUMIKIA KLABU HIYO
Mshambuliaji wa klabu ya Azam FC, Mghana, Bernard Arthur, ameamua kuvunja rasmi mkataba wa kuitumikia klabu hiyo.
Taarifa zinaelezwa kuwa Arthur amevunja mkataba kutokana na kushindwa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Aristica Cioba inayeelezwa amesafiri nje ya kimasomo.
Mshambuliaji huyo alisajiliwa na Azam chini ya Mkurugenzi wa kikosi hicho, Abdul Mohammed mwanzoni mwa msimu akitokea Liberty Professional ya Ghana.
Arthur amejiondoa Azam wakati kikosi kikijiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Jumapili ya wiki kwenye Uwanja wa Azam Complex huko Chamazi.








0 COMMENTS:
Post a Comment