Na George Mganga
Video hiyo inayokwenda kwa jina la Mvumo wa Radi aliiweka kwenye akaunti hiyo Mei 11 2018, ilionekana kwenda na SPIDI nzuri ya watazamaji, lakini ilipofika Mei 12 majira ya saa 8 kuelekea saa 9 mchana iliganda kwa muda mrefu kwa kuwa na watazamaji 781,149.
Uongozi wa Kiba kupitia LEBO yake ya RockStarAfrica ulikuja kutoa taarifa baadaye kuhusiana na kuganda kwa watazamaji hao huku LIKES na SUBSCRIBERS wakiongezeka kwenye kaunti yake ila wanaotazama video wakiwa hawapandi wala kushuka.
RockStarAfrica walieleza kuwa wanafanya mawasiliano na uongozi wa YouTube kulifanyia kazi suala hilo ambalo limewahi kuwapata baadhi ya wasanii wengine wakubwa Afrika na duniani kwa ujumla.
Leo majira ya usiku imefanikiwa kufikisha watazamaji zaidi ya milioni moja japo inakwenda kwa SPIDI ambayo ni ndogo.








:-b
ReplyDelete����������������
ReplyDelete